BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Kama unapingwa kwenye mambo yako, jifunze kitu hapa

Kwa chochote kile ambacho utaamua kukifanya hata kiwe kizuri vipi, ujue kabisa wapo watu ambao ni lazima watakupinga. Kukipinga huko hakumaanishi kitu hicho hakipo sahihi, huo ni mtazamo wao na sio wa kwako.

Kwa hiyo kuwa na msimamo kwa yale mambo unayoyafanya na usiwe mtu wa kusikiliza sana ushauri wa wengine. Unatakiwa kusimama imara kwa kujua ni kipi ambacho unatakiwa kukifanya na si kupelekwa kama upepo na ushauri wa watu.

Ukijua vizuri kwamba wapo watu ambao kazi yao ni kupinga kila kitu kwenye maisha ya wengine hutakiwi kupata tabu tena. Fata njia yako mpaka mafanikio yaonekane. Kuwa ‘master wa maisha yako’ na sio kutegemea wengine. KILA LA KHERI.

Wako rafiki katika mafanikio, Imani Ngwangwalu.

dirayamafanikio@gmail.com


Post a Comment

0 Comments