BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Kabla hujaamua kufanya jambo fulani, hakikisha unakifahamu kitu hiki

Katika ulimwengu wa sasa kwa kila kitu unachokifanya au unachotaka kufanya basi ili kitu hicho kiwe bora na chenye manufaa basi unahitaji taarifa sahihi juu ya kitu hicho. Kama unataka kufanya biashara au jambo fulani basi usikurupuke kuanza tu kufanya biashara hiyo au kitu hicho pasipina kuwa taarifa sahihi.

Kama utaamua leo kufanya jambo fulani pasina kuwa na taarifa sahihi hili lipo wazi  kwamba hautafanikiwa kwa asilia zote, kwa sababu kila wakati mambo yanabadilika sana na kama hautamua leo kuendana na mabadiliko hayo husasani katika suala la kujifunza vitu vipya basi sahau kabisa kuhusu mafanikio. 

Hivyo ninachotaka kukumbusha hapa ni kwamba kwa kuwa huu ni ulimwengu wa sasa ni ulimwengu taarifa hivyo ili uweze kuwa bora zaidi katika maisha yako unatikiwa kuwekeza muda mwingi katika kupata maarifa sahihi juu ya jambo lako ulifanyalo au unalotaka kulifanya.

Ndimi afisa Mipango, Benson Chonya
0747-030303
mafanikioapp@gmail.com

Post a Comment

0 Comments