Ulimwengu wa sasa ili uweze kukidhi mahitaji ya moyo wako yakupasa kufanya mambo yatakayokusaidia kuweza kufanikiwa kwenye kile ukipendacho hatimaye kupata amani ya moyo (peace of mind).
Ili uweze kupata amani moyo katika sekta ya mafanikio basi yakupasa kutokuwa na matatizo yatokanayo na ukosefu wa pesa, na ili uweze kuondokana na matatizo yatokanayo na ukosefu wa matatizo ya pesa basi unapaswa kuongeza mifereji mingine ya kukuingizia kipato.
Hautakiwi kutegemea chanzo kimoja cha kipato, kwani kufanya hivi kunakuweka katika ule ulimwengu ambao watu wanaoishi humo ni walalamikaji muda wote, ili uweze kujitoa katika ugumu wa maisha, uwe umejiriwa au umejiajiri yakupasa kutokutegemea aina moja ya kiingiza kipato bali unatakiwa kufikiria njia nyingi za viingiza pesa.
Ajira au kazi ya aina moja pekee haitoshi kukufanya uwe na maisha bora.

0 Comments