BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jinsi pesa zinavyopatikana kiurahisi katika karne ya ishirini na moja.

Pesa ni matokeo ya majibu ya changamoto fulani kutatuliwa. Hivyo ili uweze kupata pesa katika harakati zako za kila siku unatakiwa kuhakikisha unatafuta majibu ya changamoto ambazo zinawakabiri watu, kisha watu hao watakupa Pesa.

Kwa mfano kama eneo unaloishi, watu wa eneo hilo hutumia muda mwingi kwenda mbali na makazi yao kutafuta huduma fulani basi unachopaswa kufanya ni kuwasogozea watu hao huduma hiyo karibu.

Kila mtu anapenda urahisi katika jambo fulani, hivyo kwa kila ugumu ambao watu wananaupata katika kazi fulani katika eneo lako unaloishi basi anza kuleta majibu ya changamoto hizo . Ukifanya hili kwa umakini ni kwamba mafanikio makubwa ya kifedha yatakuwa upande wako kwani utakuwa unao uwezo wa kuona fursa mbalimbali.

Ndimi: Afisa Mipango Benson Chonya

0757-909942

bensonchonya23@gmail.com


Post a Comment

0 Comments