BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jifunze namna ya kuwa na matumizi sahihi ya akili.

Kila kitu ambacho unataka kukifanya au ambacho unakifanya basi kitu hicho huanzia katika akili. Akili ndiyo inayompa mtu nguvu na ujasiri wa kufanya jambo fulani, lakini pia akili hiyo hiyo ndiyo inayoamua kutofanya mambo ya muhimu pia.

Kutenda au kutokutenda jambo fulani hutokana na matumizi ya akili. Hivyo kila wakati ili uweze kufanikiwa katika maisha yako unatakiwa kuitumia vyema akili yako kwa sababu kama utaamua kuiruhusu akili yako iamini katika suala la kushindwa basi hata iweje ni lazima utashindwa tu.

Ila kama utairuhusu akili yako iamini kwamba utafanikiwa ni lazima utafanikiwa tu hata iweje hii ni kwa sababu aminicho mtu ndicho kitachomtokea. Amua sasa kuitumia vyema akili yako kwa kuifanya akili hiyohiyo iamini katika kufanikiwa pekee, mawazo hasi yasikae upande wako.

Mwisho naomba nikwambie ya kuwa matumizi sahihi ya akili ni mali.

Ndimi Afisa Mipango: Benson Chonya
mafanikioapp@gmail.com
0747-030303

Post a Comment

0 Comments