Miongoni mwa mambo makubwa yanayosababisha watu waendelee kuwa na maisha ya kawaida hususani katika suala la mafanikio ni tatizo la kughairisha kufanya mambo ya msingi, hili limekuwa ni tatizo kubwa sana.
Neno nitafanya baadae, nitafanya kesho, nitafanya wiki ijayo, nitafanya mwezi ujao au nitafanya mwaka ujao ndiyo chanzo kikubwa cha tatizo hili. Wengi ambao wamekuwa wakiziruhusu akili na vinywa vyao viweze kutamka maneno kama haya wamekuwa hawafanikishi kile walichokiahidi.
Wengi wamekuwa hawafanikishi kile walichokiahidi kwasababu unapopanga leo kufanya jambo fulani hapo baadae, kumbuka kama ulipokuwa unapopanga jambo hilo haukuwa na nia ya kweli, kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo hamasa ya kiutendaji inavyozidi kushuka.
Pia, watalamu wa mambo wanasema linalowezeka leo lisingoje kesho, hivyo ni vyema uitumie leo yako vyema kwa kuamua kufanya mambo ya msingi yatakayokusaidia kuweza kupiga hatua za mafanikio katika maisha yako. Amua sasa kuondokana na tatizo la kughairisha kufanya mambo ya msingi kwa kujiambia ahadi ambazo unaona unaweza kuzitekeleza.
Ndimi Afisa Mipango; Benson Chonya
0747-030303
mafanikioapp@gmail.com

0 Comments