Ili kuona kama unapiga hatua kwenye kila kitu ambacho unakifanya unatakiwa kujifanyia tathimini kama unapiga hatua au laah. Kufanya tathimini ni lazima uangalie kile ulichokipanga kukimalisha kwa wiki, juma, mwezi au mwaka kama kimefanikiwa.
Kama endapo hajafanikiwa kutimiza kile ulichojipangia kukifanya katika maisha yako basi unatakiwa kuangalia upya kitu hicho kwa umakini kwa kutazama ni wapi ambapo umekosea kisha kurekebisha yale yote ambayo ulikuwa unayakosea na kuanza kufanya upya ili uweze kufanya vizuri zaidi.
Usigope, wala kuona aibu kukosea katika kufanya yale ya msingi, kwani kukosea ni sehemu ya maisha, hivyo kama kunasehemu umekuwa ukikosea unapaswa kuanza upya kwenye mambo yako ambayo kimsingi yanakuwa hayaendi sawa, kumbuka kwamba kuanza upya kunamfanya mtu awe makini zaidi pia kukosea ni sehemu sahihi kwako ya kufanya vizuri zaidi.
Ndimi: Afisa Mipango Benson Chonya
mafanikioapp@gmail.com
0747-030303

0 Comments