Wakati nikiwa mdogo
niliwahi kusikia wakubwa wangu wakisema ya kwamba mazoea yana tabu, kwa kipindi
kile sikujua walikuwa wanamaanisha nini, ila kadri siku zinavyozidi kwenda
ndivyo ninavyozidi kuelewa walikuwa wanamaniisha nini.
Nilichokuja kukigundua
juu ya msemo huu ni kwamba mawazo ya binadamu ni mawazo ya mgando, naweza
nikasema hivyo kwa sababu akili zetu tumezielekeza katika kufanya mambo katika
mazoea. Kama mtu amezoea kula ugali muda wa mchana basi mtu huyo ukimpa wali
muda wa mchana basi utamsikia mtu huyo akisema kwa kweli mimi kula wali mchana
zijazoea.
Kwa mfano huo, angalia
watu ambao wanafanya biashara fulani
ambazo hazilipi, ukimwambia wafanyabiashara hao wafanye biashara nyingine
watatakwambia ya kwamba hawawezi kufanya biashra ambayo hawaijaizoea. Kwa
majibu ya aina hiyo ndipo nianapokubaliana na usemi ule usemao ya kwamba mazoea
yana tabu, hii ni kwa sababu watu wengi tunashindwa kufanya vitu vingine
tofauti na tulivyovizoea.
Lakini kama kweli unataka
mafanikio ya kweli ni vyema kwa jambo lolote ambalo unalifanya acha mara moja
tabia kufanya vitu kwa mazoea kwani mazoea ni dalili za uvivu, unashangaa huo
ndio ukweli ambao upo wazi. Hivyo kwa kila jambo ambalo unalifanya hakikisha ya
kwamba unatafuta mbinu nyingine za kuweza kuwa bora zaidi.
Lakini pia unashauriwa ya
kwamba Ili kufikia mafanikio zaidi ya hapo ulipo, ipo haja na ulazima wa wewe
kujituma na kufanya kazi kwa bidii sana nje ya yale mazoea uliyojiwekea. Kwa mfano,
kama umezoea kufanya kazi kwa saa 8, ongeza masaa mengine manne ya ziada. Kama
umezoea kuamka sa 12, anza kuamka saa 11 alfajiri. Fanya kitu ambacho kitakutoa
nje ya mazoea yako yaani ‘comfort zone’. Kwa
chochote kile unachokifanya, fanya nje ya mazoea yako.
Hivyo kila dakika na kila
sekunde, kama kweli unataka kuondoka katika hali uliyopo kwa sasa unachotakiwa
kukifanya kwa sasa ni kuachana mara moja ile tabia ya kuishi katika misingi ya
kimazoea (comfort zone) ambayo umeyazoea, na kufanya hivi itakusaidia sana kujenga misuri mikubwa ya
kukuwezesha kufika mbali zaidi kimafanikio.
Endapo utandokana na hali
ya kufanya vitu kwa mazoea tegemea kupata mambo makubwa ya fuatayo;
1. Utapata mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi, hii ni kwa sababu utaongeza uwezo na muda wako wa kufanya kazi.
2. Lakini pia kama utaondokana na ile tabia ya kufanya kazi kwa mazoea basi jiandae kuwa mtalamu kwa jambo ulifanyalo.
3. Faida ya tatu naomba nuongeze mwenyewe maana wewe ndiye utakaona matokeo.
Hivyo tumalize kwa kusema
ya kwamba unatakiwa kuachana mara moja tabia yako ya kufanya vitu kwa mazoe.
Tukushuru sana kila
wakati kwa kuwa sehemu ya mafundisho
haya kila siku, endelea pia
kuwashirikisha wengine.
Imeandikwa na
uongozi wa mtandao wa dira ya mafanikio pamoja na mafanikio App
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya
0 Comments