BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Amua kuwa hivi kama kweli unataka kufanikiwa

Maisha halisi ya mafanikio hujengwa na misingi imara ya mhusika mwenyewe kuweza kujitambua. Suala kujitambua linatakiwa kuanzia ndani ya mtu mwenyewe hususani katika suala la kufanya kazi. 

Maisha ya wengi yamejengwa katika misingi ya kusubiri kuambiwa ufanye nini na kwa wakati gani na mtu mwingine, Kusubiri mtu mwingine akwambie ufanye jambo fulani nawe ndipo uanze kufanya jambo hilo ni kujidanganya mwenyewe kwa sababu hautafanya kazi hiyo kutoka nafsini mwako  bali utaifanya tu ili kumridhisha mtu mwingine aliyekuambia ufanye kazi hiyo.

Ila ukweli ni kwamba hajilishi umeajiriwa au umejiajiri, kama kweli umechoka na ugumu wa maisha unayoyapitia na unataka mabadiliko makubwa ndani yako basi unatakiwa kuanza sasa kujitambua na kujitambua huku ukianza kujipangia ratiba yako ya kufanya kazi zako kwa ufanisi wa hali ya juu sana pasipo kusiburi mtu fulani akupangie au akusimamie kufanya kazi  kazi hiyo.


Ndimi Afisa Mipango, Benson Chonya
0747-030303
mafanikioapp@gmail.com

Post a Comment

0 Comments