BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jifunze Kushukuru Kwa kila jambo



Moja kati ya mambo muhimu yatakayokusaidia ili uweze kupata zaidi ya hicho ulichonacho kwa sasa ni pamoja na kuwa mtu wa kushukuru kwa kile ulichonacho au unachokipata. Nasema hivyo kwa sababu wapo baadhi ya watu wao kazi yao kubwa ni kulalamika kila uchwao.

Wengi hulalama kwa kusema mimi sina hiki, yaani sijui maisha ni magumu na manung`uniko mengine kama hayo ambayo kimsingi hayana maana yeyote ile katika maisha ya mnung`unikaji huyo. Wengi wamesahau kwamba alichonacho yeye kuna mtu mwingine hana.
Hivyo wito wangu kwako kwenye kila ambacho unakipata ili uweze kupata zaidi basi hutakiwi kuendelea kunung’unika, zaidi ya kuwa ni mtu wa kushukuru kwa sababu kuna watu wengine hawana hata hicho kitu ulichonacho wewe.
Ndimi: Afisa Mipango
Benson Chonya

Post a Comment

0 Comments