Tofauti kubwa kati ya watu wenye mafanikio na wasio na mafanikio, haipo kwenye kurithi, kipaji au uwezo mkubwa sana. Tofauti kubwa inajitokeza kwenye kufanya yale mambo ambayo yanaonekana ni rahisi.
Hili ndio tofauti kubwa inayojitokeza kati ya watu maskini na matajiri. Yale mambo ambayo yanaonekana ni madogo na ya kudharaulika kabisa wao wanayafanya bila shida yoyote na ndio yanayowapa mafanikio makubwa.
Hata ukiangalia watu wenye mafanikio na watu wasio na mafanikio wanafanya mambo yale yale ambayo yanafanana kwa siku kwa mfano kula, kusoma kitabu cha aina moja na kuhudhuria semina.
Tofauti inaanza kujitokeza hasa pale kwenye umakini wa kutumia hasa mambo yale wanayojifunza karibu kila siku. Umakini hapa sasa, ndio unawatenga waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa.
0 Comments