Nafahamu vyema wanafunzi wengi wa chuo wapo nyumbani wao wanapenda kupaita (kihomeboy).
Wengine wapo field, wengine wapo likizo. Sasa mimi leo sina shida na wale ambao wapo field, bali nina shida na wale ambao wapo likizo tu hawana field.
Sasa sikia ndugu yangu, ukiwa likizo usikae kinyonge tafuta wanafunzi waliomaliza form six kisha wasaadie kuuamplai vyuo na mikopo pia, wasaidie kujaza taarifa za lita na kuwapelekea wa wana sheria.
Baada ya hapo wakulipe hata 10,000 kwa kila mwanafunzi. Mwingine atauliza wanafunzi nitawapata wapi?
Fanya hivi, andika tangazo lako zuri lenye kusema unawasaidiawanafunzi kuomba mikopo na kuaomba nafasi kwenye vyuo mbalimbali kisha baandika matangazo hayo mtaani kwako.
Najua utapata hela nzuri tu kipindi hiki cha likizo, nimekupa mchongo huu ili usikae kinyonge ndugu yangu kwa sababu wanafunzi wengi wa form six hawajui mchongo huu kuomba vyuo, chukua fursa hiyo.
Ndimi Benson Chonya
0 Comments