Kila unachokifanya, ni lazima kiwe kina mrejesho, haijalishi ni mrejesho chanya au mrejesho hasi. Watu wengi huwa tuna tabia ya kutaka sana kupewa mrejesho chanya hasa kwa yale mambo tunayoyafanya.
Kwa mfano, kama umefanikiwa katika jambo fulani huwa tunataka kusikia sana hongera. Pongezi hizo ni nzuri, lakini ni lazima ziendane na kuambiwa ufanye tena nini ili kuboresha hicho ulichofanikiwa.
Kuishia tu kumpa mtu pongezi bila kuongeza neno la nini cha kufanya ili kuboresha kitu hicho, hiyo itakuwa ni sawa na kumpoteza. Kwa nini nasema hivyo, wapo watu ambao wakisifiwa hujisahau na matokeo yake huanza kuharibu kazi bora ya kwanza.
Tambua kila wakati PONGEZI ni nyema ikaendana na MREJESHO wa nini kifanyike ili kuweza kupiga hatua mbele za kimafanikio. Kwa kufanya hivyo, itasaidia kuweka juhudi zaidi hadi kufikia mafanikio yetu.
0 Comments