Ikiwa unapata matokeo usiyoyataka hasa kwa kile kitu unachokifanya, acha kujiona mnyonge na kukata tamaa, endelea kuweka juhudi.
Ikiwa unapitia kwenye changamoto nyingi za kimaisha pia acha kukata tamaa, endelea kuweka juhudi upo wakati ambapo utazivuka hizo changamoto hizo na kuwa huru.
Ikiwa huridhiki kabisa na mwenendo wa maisha yako na kujiona kila wakati kama mtu ambaye umepoteza, pia usikate tamaa, endelea kuweka juhudi.
Kwa kila hatua unayochukua kwenye maisha yako hata ikiwa ndogo sana, inaleta mabadiliko kwenye maisha yako.
Angalia ulikotoka kwemye maisha, sasa kwa nini ukate tamaa na wakati sasa hivi upo mbali sana? Dawa si kukata tamaa ni kuweka juhudi tena.
Hata upate matokeo mabaya vipi ambayo unaona hayakuridhishi kabisa endelea kuweka juhudi, kwani lazima juhudi zako zitaleta matunda.
Hakuna mtu katika dunia hii ambaye ameweka juhudi endelevu, halafu zikaja kumwangusha, mtu huyo hayupo.
Hivyo, hata ushindwe mara nyingi vipi, endelea kufanya mabadiliko kwenye maisha yako, kwani upo wakati mabadiliko hayo utayaona kwa wazi kabisa, hata kama kwa sasa huyaoni.
Kila hatua unayoichukua, kumbuka inakusogeza karibu kabisa na mafanikio yako. Chukua hatua sahihi, ili ufikie mafanikio yako.
0 Comments