Kama kuna kitu unakifanya, kifanye kitu hicho kwa nguvu zote na amini kuwa kitafanikiwa kwa asilimia kubwa. Acha kujaribu kuruhusu mawazo ya kutokufanikiwa hata kidogo ndani yako.
Hakuna mtu ambaye anaweza kuamini sana jambo unalolifanya kuwa litafanikiwa, zaidi yako. Wewe ndiye unatakiwa uwe wa kwanza kuamini hivyo.
Hata ikitokea wengine waseme sana kwamba jambo unalolifanya haliwezi kukufanikisha, kwa kuwa umeshaamini inawezekana, hutasimama kufanya jambo lako.
Amini juu ya fursa unayoifanya, amini juu ya mafanikio yako kwamba kwa vyovyote vile liwe jua au mvua lazima ufanikiwe na itakuwa hivyo. Hakuna atakayeweza kukuzuia katika hilo.
Narudia tena, kwa chochote kile unachokifana, ukiamini kwamba kinaweza kufanikiwa uwe na uhakika kitafanikiwa. Mafanikio makubwa yanajengwa kwa kujiamini kwanza ndani yetu, kuwa tunaweza.
0 Comments