Kupata mafanikio sio kazi rahisi kunahitaji nguvu na jitahada nyingi sana hadi kufikia kule unakotaka kufika kimafanikio.
Kuna wakati utakatishwa tamaa, kuna wakati utaambiwa huwezi hili au lile, lakini yote hayo yanapotekea yasikukatishe tamaa jipe moyo na endelea kusonga mbele.
Hata Jesca Cox, alikatishwa sana tamaa na wengi na kuambiwa asingiweza kutumiza ndoto yake ya kuwa rubani eti kwa sababu ya ulemavu wake wa mikono.
Leo hii, Jesca ni rubani wa kwanza duniani ambaye hana mikono, je, jiulize nini kinachokukwamisha wewe? Endelea kupambana na songa mbele.
USIKATISHE NDOTO YAKO KWA SABABU TU YA MANENO YA WATU.
0 Comments