Katika maisha yako, anza kujenga utaratibu mpya wa kujiuliza maswali kwa mambo unayoyataka yawe katika maisha yako. Kwa mfano, unaweza ukawa unajiuliza ninafanyaje ili niingize kipato kikubwa zaidi au ninafanyaje ili niweze kutoka hapa nilipo.
Akili kama akili imeumbwa ili ikusaidie kutafuta majibu kwa yale mambo magumu. Sasa kama upo upo huisumbui akili yako ikusaidie kutatua changamoto zako, aisee uwe na uhakika utabaki sana hapo ulipo.
Kumbuka kila wakati akili ya binadamu, inafanya kazi kwa kuuliza maswali na kujijibu. Chochote ambacho unajiuliza sana kwenye akili yako haijalishi ni kibaya au kizuri, ni lazima utakipata.
Acha kukukosea katika hili, jiulize maswali magumu yatakayosaidia kuboresha maisha yako. ukiisumbua akili yako, utapata hicho unachokihitaji na utajenga msingi wa maisha bora sana kwako na kizazi chako cha baadae.
0 Comments