Zipo alama ambazo umewekewa na jamii yako na alama hizo kuna wakati zinakupoteza sana. Kwa mfano, umeambiwa na kuwekewa alama kwamba wewe ni mjinga, huwezi kitu, ni maskini na pengine hufai.
Lakini katika uhalisia ulivyo, wewe hauko hivyo kama jamii ilivyokupachika alama hizo. Wewe ni mtu wa mafanikio ikiwa utalielewa hilo na kuchukua hatua sitahiki ambazo zinaweza kubadilisha maisha yako na kufutilia mbali alama hizo.
Usijaribu kuamini kila ambacho unaambiwa, ikiwa utaamini hizo alama ambazo unapewa na jamii yako tambua hutaweza kufanya kitu chochote. Utabaki hapo ulipo na kuumia sana.
0 Comments