Kitu chochote katika maisha yako unaweza kukibadili kama ikiwa utakifanyia mazoezi makubwa kila siku na bila kujali unapata ugumu au shida kiasi gani. Unaweza ukabadili hali ya tabia yako au kitu chochote kile kinachokusumbua.
Kwa mfano, kama unataka kubadili tabia fulani hivi mbaya, tuchulie kuchelewa kuamka asubuhi, inabidi ujizoeze kuamka saa moja kabla kila siku. Kwa mwanzo itakuwa ngumu sana kwako, lakini endelea kufanya hivyo mpaka itafika wakati utazoea.
Tabia yoyote au kitu chochote unachotaka kukibadili inabidi ukifanyie mazoezi sana. Ikiwa hautafanya hivyo na ukategemea ukapata urahisi basi ni lazima utashindwa. Kubadili tabia sio kazi rahisi kama mwanzoni hutaweka juhudi hadiakili izoee.
0 Comments