BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

 


Uzoefu katika maisha yako hauji kwa bahati mbaya, bali unakuja kwa kuweka nguvu nyingi za uzingativu (Focus) hasa kwa kile kitu unachokifanya kwa muda mrefu. Ukitaka kuwa mtaalamu uliyebobea katika jambo fulani, weka nguvu za uzingativu katika jambo hilo bila kuacha kila siku na utalifanikisha.

Unaposikia ‘aisee fulani ni mzoefu wa kazi yake na inampa mafanikio,’ tambua sio uzoefu wa miaka ila ni uzoefu wa kitaalamu. Unaweza ukawa katika kazi yako kwa muda mrefu ila kama hujifunzi, utakuwa sawa na mtu aliyeanza hiyo kazi leo.

Jenga uzoefu kwenye kazi yako kwa kuamua kuweka nguvu za uzingativu hapo na kujifunza kwa uhakika. Hakuna ambacho utakikosa sana ikiwa utaamua kuweka nguvu zako nyingi kwa kile unachokifanya na kuacha kuruka ruka.


Post a Comment

0 Comments