Acha kuuchanganya ubongo
wako kwa kuupa vitu ambavyo huvihitaji. Kwa lugha rahisi waza vitu ambavyo unavihitaji katika
maisha yako. Tofauti na hapo utakuwa unajichanganya sana kwa kuufanya ubongo
wako ushindwe kuelewa kipi unachokitaka na kipi hukitaki.
Unataka mafanikio tulia,
tambua ni kipi unachokitaka na ukifanyie kazi hicho kila siku. Ila ukiwa ni mtu
wa tamaa mara unataka hiki mara kile itakupelekea
kupata matokeo ambayo siyo sahihi katika maisha yako na usishangae ukishindwa
kufanikishakaribu kila kitu. kumbuka kila wakati Contradicting desires create contradicting results.
0 Comments