Kama
una lengo la kujiongezea kipato, acha kuogopa kufanya kitu chochote. Kama kuna
kitu fulani ambcho unatakiwa ukiuze, hebu uza kitu hicho. Acha kujisikia vibaya
kwa sababu unauza kitu fulani eti ambacho hakina hadhi yako.
Maisha hayataki aibu. Fanya kitu chochote cha kukukiingizia kipato ilimradi kitu hicho kiwe halali na hakiwaumizi wengine. Maisha ya kuona aibu kufanya jambo fulani yatakufanya uzidi kukosa pesa kila kukicha na mwisho wa siku utajikuta umekuwa mlalamikaji.
Acha
kuwa na ndoto za kufanya mambo makubwa saana na halafu ukadharau kufanya hata
vidogo ambavyo huna. Kumbuka, jiwekee ndoto kubwa sana lakini anza na hapo
ulipo, anza na kidogo ulichonacho. Hutaki kufanya hivyo, jiandae kuishi kwa
ndoto na hutaweza kufanikiwa.
0 Comments