Ni
rahisi kufanikiwa na kupata karibu kila kitu unachokihitaji katika maisha yako
ikiwa utakuwa tayari kuwasidia wengine nao kuweza kufanikiwa. Ndio maana mara
nyingi watu wenye mkono wa ‘birika’ si
rahisi sana kuweza kuwaona wakifikia viwango vya mafanikio makubwa.
Jiulize
kitu gani ulichonacho ambacho unaweza ukakitoa na kikawa msaada mkubwa kwa
wengine? Kama kitu hicho unacho hebu kitoe, acha kukaa nacho tu wewe peke yako,
washirikishe na wengine ili kiwe baraka kwenu wote.
0 Comments