BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Ugumu wa kila jambo hutatuliwa hivi.

Unapotaka kufanya jambo fulani lenye kuleta manufaa kwako basi jitahidi sana kutafuta mwalimu atakayekuelekeza namna sahihi kulifanya jambo hilo.

Kitu ambacho unakiona ni kitu kigumu kwako kumbuka kuwa kuna mtu kitu hicho kwake ni chepesi, hivyo mtafute mtu huyo aweze kukusaidia ili nawe uweze kukijua kitu.

Kama unataka kuwa mbombezi katika kilimo cha nyanya, basi tafuta mtu ambaye alikwisha fanya jambo hilo kwa vitendo ili awe anakupa mwongoza wa kitu gani cha kufanya na kitu gani si kufanya.

Kama utakuwa bingwa wa kusuka aina nzuri za mitindo ya nywele, usijione mnyonge bali tafuta msusi anayejua kusuka mitindo hiyo akusaidie ili nawe uweze kujua kusuka.

Kuendelea kukaa na kuendelea kusema napenda kufanya kitu fulani bila kutafuta mtu atakayekusaidia ili nawe uweza kujua kitu hicho ni kazi bure kwako.

Bali unapaswa kutafuta mwalimu anayejua jambo unalolitaka kulijua ili akufundishe jambo hilo.

Ni muhimu sana kuwa mwalimu m-bobezi kwa sababu yeye anakuwa anajua changamoto ambazo akikuleza vyema inakuwa ni rahisi kwako kuepukika.

Tafuta mwalimu akusaidie kufikia lengo lako usikae kinyonge, bila kuwa na mwalimu vipo vingi utakuwa unakosea ili ukiwa na mwalimu utaepuka vingi.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments