Umakini kwenye kila jambo lolote lile ndiyo majibu sahihi ya kile ukifanyacho. Huwezi kusema unataka mabadiliko chanya kwenye jambo fulani wakati huo huo umakini wako umeuacha nyuma, hiyo itakuwa ni kazi bure yaani ni sawa na kumuacha ng'ombe mwenye njaa kali akulindie majani.
Maana yangu ni hii, umakini ndiyo chachu iletayo mafanikio yako, haijalishi ni changomoto kiasi gani ambazo unakatuna nazo, hata ziwe kubwa kiasi gani, unachopaswa kuelewa ni kwamba umakini wako wa kutotoka nje ya malengo yako ndiyo utakaokupa mafanikio uyatakayo.
Kwa nukta hiyo unachopaswa kukumbuka juu ya mafanikio makubwa uyatakayo ni kwamba mafanikio hujengwa na umakini wako katika jambo ulitakalo.
Ndimi afisa Mipà ngo Benson chonya.
0747-030303
0 Comments