Kama unafanya kazi yoyote ile acha kufanya kazi hiyo kinyonge, acha kufanya kazi hiyo kwa kuamini kwamba utaenda kupata matokeo hafifu au matokeo ya chini, fanya kazi yako kama mshindi na usiogope kitu.
Ukienda kufanya kazi yako kwa kuamini utashinda, basi utaweza kushinda kweli. Ni hatari sana kufanya kazi zako kinyonge kwa kuamini umeshindwa, kwa hiyo unafanya ili usukume siku, ogopa sana hiyo kitu maishani mwako.
Watu wengi wanafanya kazi zao kwa mtazamo wa kinyonge, wanafanya kwa kuamini kwamba mambo yameishia hapo na hawawezi kufanikiwa pa kubwa, huo ni mtazamo hatari ambao unawapoteza kabisa.
Ili kufanikiwa, acha kabisa kufanya kazi kinyonge. Kazi yoyote ifanye kishujaa. Usiione ni kazi ya washindwaji, ona ni kazi ya kukufanikisha, na acha kuidharau hata kidogo inayokupa kula yako ya kila siku.
Ukiifanya kazi yako kishujaa na kuipa heshima, utafanikiwa.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
0 Comments