BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Ifahamu Misingi Hii Ya Kuilea Ndoto Yako ili Uweze Kufanikiwa.


Katika ulimwengu huu wa teknolojia kila mmoja wetu ana ndoto yake, na kila miongoni mwetu anatamani siku moja ndoto iwe kweli. Ila changamoto kubwa huwa inakuja ni kwa jinsi gani unaiweza kuifanya ndoto hiyo kuwa kweli. Wengi wetu ndoto zetu ni za mdomoni tu, huwa hazina uhalisia wa jinsi ya kuzikamilisha ndoto hizo.

Lakini siku zote ikumbukwe katika safari ya mafanikio, kuwa makini sana na jinsi unavyoitunza na kuilea ndoto yako. Kama ndoto yako unaitunza na kuilea katika hali ya hofu na mashaka sana basi, utavuna magugu na hautaweza kufanikiwa.

Wengi wetu tumekuwa tumeweka mitazamo hasi juu ya ndoto zetu, wengi tumekuwa tukiyataza mambo katika mtazamo hasi, wengi tumekuwa hatujui namna na jinsi ya kuzitimiza ndoto zetu. Kwa mfano unaweza ukakuta mtu anatamani kuwa mfanyabiashara Fulani, lakini cha ajabu ukimuuliza mtu huyo ni mikakati gani ambayo amejiwekea ili kukamilisha ndoto yake hiyo, utakuta hakuna mkakati hata mmoja. 

Najaribu kujihoji kwa sauti ya nne, hivi kwa kufanya hivyo ni kuijenga ndoto yako au ni kuobomoa? Bila shaka kufanya hivyo ni kuibomoa ndoto yako na hatimaye kujiandalia makazi ya kiumaskini.

Lakini ukweli ni kwamba ili uweze kutimiza ndoto yako unatakiwa kuitunza na kuilea ndoto hiyo katika misingiya  imani na matumaini makubwa ya kimafanikio, lakini pia ni lazima uweze kujiamini kila wakati, hii ni kwa sababu wapo wengi wanaoshindwa kufikia ndoto zao kwa sababu ya kuzielea ndoto zao katika mazingira mabovu.

Kama ulivyo mmea ili ukue ni lazima umwagaliwe maji safi, halikadhalika ndoto  yako iko hivyo hivyo. Ni lazima ndoto yako ituzwe kwa matumaini na imani ya mafanikio na sio kuitunza katika hofu na woga ambapo mwisho wa siku ni lazima utakwama.

Hivyo kwa kuwa wewe ndiye mmliki wa ndoto yako hakikisha unaweka mikakati imara ambayo itakufanya uweze kufika pale ambapo unapopataka, kwani endapo utafanya kinyume chake ni kushindwa kutimiza  kutimiza kusudio lako hapa duniani.

Hivyo kila wakati jaribu kutafakari juu ya mambo haya;

Najua hapo ulipo una ndoto ya aina fulani, jiulize 

Unailea ndoto yako katika mazingira yapi? 

Je, unajiamini  ya kwamba utafanikisha ndoto yako? 

Au  upo kwenye mazingira ya mashaka na hofu? 

Lakini ikumbukwe ya kwamba mazingira yoyote yale unayoyatumia kuilelea ndoto yako yanakupa jibu kama utafanikiwa au hautafanikiwa kuifanikisha ndoto yako. Hivyo ni vyema ukatafakari kuhusu mazingira uliyopo kwa sasa kama ni kweli ndoto yako itatimia au haitatimia

Imeandikwa na uongozi wa mtandao wa dira ya mafanikio pamoja na Mafanikio App

Imani Ngwangwalu & Benson Chonya



Post a Comment

0 Comments