BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jifunze kuchukua hatua stahiki kwenye kila jambo


Miongoni mwa vitu vitakavyokusaidia sana kuweza kupiga hatua za mafanikio katika maisha yako ni pamoja na kuchukua hatua stahiki kwenye kile unachokifanya.

Kama umeamua kufanya jambo fulani basi unatakiwa kufanya sana jambo hilo kwa kiwango kinachostahili, usifanye kitu fulani eti kwa sababu unataka kuwafurahisha watu, wala usifanye jambo fulani eti kwa sababu unajaribu.
Kufanya kitu chochote kwa sababu hizo ambayo nimezieleza ni kupoteza muda bure. Dhamira na nia ya kufanya jambo lolote katika maisha yako itoke nafsini mwako.
Ukifanya jambo lolote ambalo nafsi yako haijaridhia kulifanya jambo hilo ni kwamba jambo hilo halitafanyika kwa ustadi pia hata matokeo yake yatakuwa ni kiduchu pia.
Hivyo amua sasa kuruhusu moyo na akili yako kuweza kuchukua hatua stahiki kwa yale unayoyajua kisha kuyaweka katika matendo, pia uyafanye kwa kuyapenda kutoka nafsini mwako, kufanya hivi itakusaidia sana kuweza kupiga hatua za maendeleo yako binafsi na watu wengine.
Ndimi ; Afisa Mipango Benson Chonya

Post a Comment

0 Comments