BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mambo makubwa mawili unayopaswa kuyafahamu katika safari yako ya kimafanikio

1. Kujitoa.
Ili kuona unapata mafanikio makubwa hakikisha ya kwamba unajitoa kwa moyo wote katika kupata kile unachokiahitaji. kitu chochote unachofanya jitoe kukipenda kitu hicho. Kwa mfano kama wewe ni mfanyabiashara eneo fulani hakikisha unaipenda kazi yako kwa kujifunza kila siku vitu vipya juu ya jambo unalolifanya kila wakati.

Kama wewe ni mfanyabiashara hakikisha ya kwamba unajua hali ya ushindani inavyokwenda katika sokoni. Lakini pia Hakiksha unafanya jambo lolote kwa juhudi zote nakuhakikishia utapata kile unachokihitaji. mara nyingi usifanye kitu kwa kusema unajaribu ila ni lazima ujifunze kujitoa kweli kweli.

2. Uvumilivu.
Wengi wetu huwa hatuna hata chembe ya uvumilivu katika kuyasaka mafanikio, hasa pale changamoto zinapojitokeza katika mambo tunayofanya, wengi tumesahau ya kuwa changamoto ni sehemu anayopitia mtu yeyote msaka mafanikio, kwa maneno mengine tunaweza sema ya kwamba changamoto huwa hazikwepeki kwa msaka mafanikio.

Hivyo Jambo la msingi la kuzingatia ili uweze kufika mbali ni vile ambavyo utaweza kuwa uvumilivu na siyo kukata tamaa. Kuna usemi wa wahenga unasema mvulivu hula mbivu hivyo tuishi usemi huu kwa kufanya kazi kwa bidii na kuzikubali changamoto na kujua jinsi gani ya kuziepuka changamoto hizo ili tupate mafanikio tunayoyahitaji.

Endelea kutembele MAFANIKIO APP kila wakati.

Post a Comment

0 Comments